Alhamisi , 8th Sep , 2022

Malkia Elizabeth II wa Uingereza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96, Kasri la Buckingham limetangaza 

Malkia Elizabeth II, wa Uingereza alitawala kwa muda mrefu zaidi ambapo  utawala wake ulidumu kwa miongo saba

Elizabeth aliingia madarakani  mwaka 1952, baada ya kifo cha baba yake, Mfalme George VI. 
Malkia Elizabeth II amefariki  katika Kasri la Balmoral huko Scotland baada ya madaktari kusema walikuwa na wasiwasi kuhusu afya yake 

Kutokana na kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza mwanae Prince Charles mwenye miaka 73 ataiongoza nchi katika maombolezo wakati akisubiri kuthibitishwa kuwa mfalme mpya