Mama Wema aingilia mahusiano ya mwanae, aweka nia

Jumatano , 3rd Apr , 2019

Mama Mzazi wa Muigizaji Wema Sepetu, amesema akiwa kama mzazi wa muigizaji huyo, amechoka na vitendo vya muigizaji Diana Kimary kwa kuwa anamrudisha nyuma mtoto wake kiasi cha kushindwa kufanya maendeleo.

Wema Sepetu akiwa na Diana Kimary

Kupitia sauti zainazotembea mitandaoni zikidaiwa ni za mama yake Wema, mzazi huyo amesema kwamba uchungu wa Wema anaufahamu yeye na ndiyo maana hataki kumuona mwanaye akiwa pamoja na Diana.

Amesema kwamba wakati wa matatizo ya Wema yeye ndiye huwa anateseka peke yake wakati hao kina Diana wakiwa mbali huku akisisitiza hakuna la maana wanalofanya wala kumshauri Wema jambo la maana.

Mama wema amesema atakula sahani moja na Diana kuhakikisha anamtenganisha na Wema kwani anaamini nazi haiwezi kushindana na jiwe.

"Huyo Diana nimeshampiga nitaendelea kumpiga mpaka nihakikishe namvunja mguu", imesema sauti hiyo inayodaiwa kuwa ni ya mama Wema.

Pamoja na hayo mama wa muigizaji huyo amewataka mashabiki na watu wa karibu wa Wema wamuambie ukweli kuhusu matendo anayoyafanya hata kama atawachukia.