Jumanne , 13th Dec , 2022

 Marekani imewawekea vikwazo vya kifedha Raia wanne wa Zimbabwe akiwemo mtoto wa rais Emmerson Mnangagwa.

Rais Mnangagwa na mwanae wote wamewekewa vikwazo na Marekani.

 

Inamshutumu Emmerson Mnangagwa Junior kwa kuhusishwa na mfanyabiashara , Kudakwashe Tagwirei, ambaye tayari yuko chini ya vikwazo vya Marekani kwa shutuma za ufisadi.

Marekani  inasema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Bw.Tagwirei ametumia mchanganyiko wa shughuli za kibiashara na uhusiano wake unaoendelea na rais kukuza himaya yake ya kibiashara kwa kiasi kikubwa na kuingiza mamilioni ya dola.

Rais Mnangagwa tayari yuko chini ya vikwazo vya Marekani.

Katika taarifa yake, Wizara ya Fedha imeitaka serikali ya Zimbabwe kushughulikia kile ilichokiita   magonjwa mengi nchini humo ikiwa na maana ya matatizo, ikiwa ni pamoja na wasomi wafisadi wanaozinyanyasa taasisi kwa manufaa yao binafsi.