Jumamosi , 25th Jan , 2020

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Ummy Mwalimu, amekemea watu wanaowatenga watu wenye ugonjwa wa Ukoma, kwakudhani kwamba wanaweza kuwaaambukiza kwa kusogeleana kitendo ambacho si kweli kwa mujibu wa wataalamu wa afya.

Waziri Afya Ummy Malimu akiwa na DC wa Dodoma Mjini Patrobasi Katambia lkatika Kijiji cha Msamalia ambacho wanaishu watu wenye Ukoma

Ameyasena hayo leo mkoani Dodoma katika Kijiji cha Msamalia ambapo ipo kambi ya wagonjwa wa Ukoma na kusema asilimia 50 ya wagonjwa wa ukoma hupatwa na ugonjwa wa Sonona kutokana na kunyanyapaliwa na jamii.

Kwa upande wake Bibi Beatrice ambaye anaishi kwenye kambi hiyo ya waathirika wa ugonjwa wa Ukoma ameishukuru Serikali kwakuwakumbuka kwa kuwapelekea vyakula.

Kesho ni siku ya Ukoma duniani na kauli mbiu inasema kuwa 'Tuthamini haki utu wa waathirika wa Ukoma, kwa kutokomeza ubaguzi unyanyapaa na chuki'