Ijumaa , 19th Apr , 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amepiga marufuku wananchi wa mkoa huo kuanza kunywa pombe asubuhi badala ya kufanya shughuli za maendeleo na za kiuchumi hali ambayo inaweza kusababisha kudumaa kwa shughuli za kiuchumi kwa wananchi.

Halima Dendego, Mkuu wa Mkoa wa Singida

Mkuu wa mkoa ametoa kauli hiyo leo Aprili 19, 2024 katika kijiji cha Kashangu, Halmashauri ya Itigi kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Elimu na Afya (PAUSE)

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa mkoa huo, Dkt. Fatma Mganga amewataka watendaji wa halmashauri na kata kusimamia vizuri ujenzi wa miradi ya maendeleo hasa umaliziaji wa majengo mbalimbali ili kudhibiti vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi.

Amesema hatapenda kusikia wala kuona wizi wa vifaa katika miradi ya maendeleo hivyo viongozi lazima wasimamie kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi na sio vinginevyo.