Jumamosi , 21st Sep , 2019

Leo Septemba 21, 2019, limefanyika tamasha la Arabian Dreams, ambalo lilikuwa na mashindano ya kukimbiza Mbuzi maarufu kama "The Goat Races" katika viwanja vya Green Kenyata Oysterbay Masaki Jijini Dar es salaam.

Mmoja wa washindi wa mbuzi

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital Meneja mahusiano wa shindano hilo Abdallah Singano, "Tunafungua kambi ambazo watu hufanya vipimo bure vya Afya na kama ukigundulika unatatizo lakiafya tunakupeleka hospitali".

Singalu ameongeza kuwa wanakusanya viingilio vinavyotolewa na watu ambavyo hutumika katika kuinua mfuko wa Routes Oysterbay, ambao husaidia kuwaendeleza wanafunzi wa vyuo vikuu Nchini waliopata nafasi ya kusoma na kushindwa kulipa ada. Pia husaidia huduma za Afya kwa kuweka kambi za vipimo na watu kupima bure na kupatiwa matibabu.

Mashindano hayo ya Mbio za Mbuzi ni moja ya Burudani, ambayo huweka Familia pamoja, kuwepo kwa burudani tofauti tofauti na sehemu zilizoandaliwa kwaajili ya Watoto, vyakula na michezo mingine mingi.