Askofu Gwajima akifuatilia mchakato wa kura za maoni mapema kabla ya matokeo kutangazwa
Jimbo hilo lilikuwa na jumla ya watia nia 170 huku wajumbe wenye sifa za kupiga kura walikuwa ni 475.
Dominic Jacob amefuatiwa na Angella Kiziga ambaye amepata kura 85 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Askofu Josephat Gwajima 79.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta ameshika nafasi ya 4 kwa kupata kura 61, huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kabla ya kuhamia CCM mapema mwaka huu Vincent Mashinji amepata kura 2.
#Uchaguzi2020 Zoezi la kura za maoni katika Jimbo la Kawe Dar es salaam CCM, limemalizika na Furaha Dominic Jacob ameongoza kwa kupata kura 101.
Furaha Dominic Jacob - 101
Angella Kiziga - 85
Josephat Gwajima - 79
Benjamin Sitta - 61
Vincent Mashinji - 2 pic.twitter.com/9OS8ERjBbS— EastAfricaTV (@eastafricatv) July 21, 2020




