Jumatatu , 13th Oct , 2025

Vita vya Israel dhidi ya Gaza vimeua watu wasiopungua 67,806 na kujeruhi 170,066 tangu Oktoba 2023. Jumla ya watu 1,139 waliuawa nchini Israeli wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7, 2023, na karibu 200 walichukuliwa mateka.

Mamia ya watu waliokuwa wakishangilia wamekusanyika katika uwanja wa Mateka wa Tel Aviv huku jeshi la Israel likisema kuwa limewapokea mateka 20 baada ya kusafirishwa kutoka Gaza na Magari ya Msalaba Mwekundu.

Hamas imewaachilia mateka wote 20 wa Israel waliokuwa wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu wanasubiri kuachiliwa kwa karibu watu 2,000 kutoka jela za Israel kama sehemu ya makubaliano hayo.

Wakati huo huo tayari Rais wa Marekani Donald Trump amewasili Israel, na anahutubia bunge la Israel Knesset na anatarajiwa kuongoza mkutano wa kilele nchini Misri kuhusu makubaliano hayo.

Wapalestina wanaendelea kurejea katika magofu yaliyosalia kwenye maeneo ya makazi yao kaskazini mwa Gaza huku msaada wa kibinadamu unaohitajika sana ukianza kumiminika katika Ukanda huo.