Polisi wanasema washukiwa wawili wanashikiliwa, huku mshukiwa mmoja akikamatwa katika eneo la tukio na afisa ambaye hakuwa kazini, na kwamba kwa sasa hakuna mtu mwingine anayetafutwa.
Tukio hilo lilitokea Jumatano katika jengo la Cielo Vista Mall, ambalo lipo karibu na duka kubwa la Walmart ambapo watu 23 waliuawa katika shambulio la ubaguzi wa rangi mnamo 2019, moja ya mauaji mabaya zaidi ya risasi katika historia ya Marekani.
Waathiriwa wote wanne walikuwa wanaume huku Majeruhi wawili wanasemekana kuwa katika hali mahututi.
Wiki moja iliyopita mtu mwenye silaha katika shambulio hilo, Patrick Crusius, alikiri makosa 90 ya wakati akihojiwa kuhusiana na uhalifu wa chuki na makosa ya silaha za moto.
Hilo linajiri katika kipindi ambacho Jumatatu wiki hii, wanafunzi watatu waliuawa na wengine watano kujeruhiwa baada ya mtu mwenye silaha kufyatua risasi katika chuo kikuu cha jimbo la Michigan



