Mahakama kuu mwezi uliopita ilimtangaza Degamo kuwa mshindi halali wa kinyang'anyiro cha ugavana wa Negros Oriental
Polisi walisema washukiwa sita waliokuwa wamebeba bunduki na kuvaa sare sawa na zile zinazovaliwa na huduma za silaha waliingia nyumbani kwa gavana huyo katika mji wa Pamplona na kufyatua risasi.
Kwa muhibu wa mjane wa gavana huyo Janice Degamo, ambaye pia ni meya wa Pamplona, amesema mumewe gavana wa jimbo la Negros Oriental , Roel Degamo, hakustahili kifo cha aina hiyo kwani likuwa akiwahudumia wapiga kura wake siku ya Jumamosi
Polisi wamesema katika taarifa yao ya leo kwamba hali ya waathiriwa waliolazwa hospitalini haijulikani.
Degamo, mwenye umri wa miaka 56, ndiye mwanasiasa wa hivi karibuni kulengwa katika historia ndefu ya Ufilipino ya mashambulizi dhidi ya wanasiasa, na anakua ni wa tatu kupigwa risasi tangu uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana.
Rais Ferdinand Marcos alilaani kile alichokitaja kama mauaji ya mshirika wa kisiasa Degamo na kuahidi kuleta haki ya haraka kwa wauaji wake.




