Jumatatu , 1st Aug , 2016

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana na Ajira, Anthony Mavunde,amewataka vijana nchi kuachana tabia ya kutopenda kufanyakazi na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana na Ajira, Anthony Mavunde.

Mhe. Mavunde amesema hayo Mjini Lindi, wakati wa mahafali ya kwanza ya mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi kwa vijana wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi katika manispaa ya Lindi.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa wanapaswa kutumia fursa kama hizo za mafunzo ya ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi huku akiwataka vijana kuacha kukataa tamaa wakati wakiwa kwenye harakati za utafutaji.

Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Simon Ndembeka, amesema lengo la mradi huo ni kuondoa hali ya umasikini kwa vijana ambao wamezingirwa na hali ngumu na wanaishi katika mazingira hatarishi ya kuweza kufanya uhalifu au kuingia katika matumizi ya madawa kwa sababu ya kukosa ajira.

Wakizungumza mara baada ya Mahafali hayo baaadhi ya vijana hao 150 waliohitimu mafunzo hayo wameushukuru mradi na kusema umewasaidia kujiwezesha kimaisha na kuanza kujitegemea kwa kutumia biashara walizozianzisha kupitia mradi huo.

Sauti ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana na Ajira, Anthony Mavunde.