
Rukia Kisengo (63), mjane aliyedhulumiwa eneo
Waswahili wanasema chozi la mnyonge malipo kwa Mungu, ujumbe huu unadhihirisha yaliyojificha ndani ya moyo wa mama huyu mjane ambaye anasema aliondoka kijijini hapo na kwenda Dar es Salaam kwa watoto wake kwa ajili ya matibabu na aliporejea akakuta shamba hilo tayari limeuzwa, shamba ambalo amelimilika kwa miaka 30 sasa.
Kwa upande wao mashemeji na wifi wanaodaiwa kudhulumu eneo hilo, wamesema kwamba eneo hilo ni la kwao na walilipata tangu serikali ya awamu ya kwanza.