Ijumaa , 21st Dec , 2018

Hatma ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambapo sasa wataendelea kuwa rumande hadi Januari 3, 2019 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha kesi yao.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Uamuzi huo wa mahakama umekuja katika kesi inayowakabili viongozi wakuu wa Chama hicho, wakiongozwa na Mweneyekiti huyo wa CHADEMA na baadhi ya viongozi wenzake wa juu pamoja na wabunge, ambapo kesi hiyo iliitwa leo kwa ajili ya kutajwa na kwa uamuzi huo wa mahakama, viongozi hao watasheherekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya wakiwa gerezani.

Kwa mujibu wa wakili wa serikali, Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea mahakama ya Rufaa hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Kwa upande wake, wakili wa upande wa washtakiwa Faraja Mangula walieleza baadhi ya Mawakili akiwemo Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange Januari 4, 2019.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama, Mbowe na Matiko wamerudishwa gerezani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 23, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana ikiwemo kutoka nje ya nchi bila kibali.