Ijumaa , 11th Oct , 2019

Mbunge wa Viti maalum, kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM, anayewakilisha kundi la Vijana Mkoa wa Kagera, Halima Bulembo, amesema moja ya mambo ambayo kwake hayazingatii ni kuhusu kipato cha mwanaume anayetaka kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi na kwamba yuko tayari kuwa na mtu asiyekuwa

na kazi ila anachoangalia ni uchapakazi wake tu.

Halima Bulembo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni, kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana.

''Mimi naweza kuishi na mtu ambaye hajasoma na asiye na hela, lakini awe ni muhangaikaji, anaweza kuuza chipsi, kuuza maji na vinginevyo, ili mradi watoto wanajua anatoka asubuhi anaenda kufanya kazi" amesema Halima Bulembo.

Tazama mahojiano kamili hapo chini.