Ijumaa , 10th Dec , 2021

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Ngonyani Msongozi, amegawa vyerehani, majiko ya gesi, chupa za chai pamoja na mbegu za alizeti kwa wanawake wa wilaya ya Namtumbo vitakavyowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na suala la utegemezi.

Baadhi ya wanawake waliokabidhiwa vyerehani na chupa za chai, kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi

Mbunge Msongozi amesema kwamba wanawake wengi wamekuwa tegemezi kwa kushindwa kujishughulisha, hivyo ameamua kuwaletea vyerehani hivyo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kaulimbiu ya Tanzania ya viwanda kwa kuwainua wanawake.