Mbunge amtaja atakayempa kura ya Urais

Alhamisi , 10th Oct , 2019

Mbunge wa Vijana wa kutokea Mkoa wa Kagera, kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Halima Bulembo, amesema akipewa nafasi ya kuchagua kati ya viongozi 4, akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani, William Lukuvi, Paul Makonda pamoja na Polepole, amesema yeye atamchagua MaMA Samia kushika

kurithi kiti cha Rais Magufuli akimaliza wakati wake.

Mbunge Bulembo ametoa kauli hiyo wakati akizingumza kwenye kipindi cha Kikaangoni, Kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, wakati akijibu swali kwa mtazamo akipewa nafasi ya kumtaja anayefaa kurithi kiti cha Rais Magufuli, ambapo amesema anadhani Mama Samia anaweza kuchukua nafasi hiyo.

Bulembo amesema moja ya sababu ya kumchagua Mama Samia, ni kutoa morali kwa wanawake kushika nafasi za juu ambapo amesema "kati ya hao uliowataja mimi nikipewa nafasi ya kuchagua mtu anayefaa kumrithi Rais Magufuli ni Mama Samia, kwa sababu mwanamke ambaye ni mfano bora sana."

"Mimi moja ya nafasi ambazo ninandhani nitagombea nikifika miaka 40, ni kuwania Urais kwa tikei ya Chama Changu, kwa sasa nina miaka 28, nadhani nikifika huko nitafikiria" amesema Bulembo.

Je unahitaji kuwekeza kwenye miradi ya Serikali, na ukapata faida ya kama yote, basi UTT AMIS ni sehemu sahihi

UTT AMIS hii ni Kampuni inayohusika na uendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja, na pia inatoa huduma za usimamizi wa mitaji binafsi na kwa sasa inasimamia mifuko mitano ambayo ni UMOJA, WEKEZA MAISHA, WATOTO, JIKIMU NA UKWASI.
 

Na hivi sasa UTT AMIS inakuletea mfuko wa BOND FUND, huu ni mfuko uliowazi unaowekeza katika masoko ya hati fungani za Serikali, hati fungani za Makampuni na katika masoko ya fedha, mfuko huu una faida lukuki ambapo unaweza kuwekeza kwa kiwango cha chini cha kuanzia  sh. 50,000/-

Kwa maelezo zaidi piga namba za bure 0754 800 544, 0715 800 544