
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Songwe Neema Gerald
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo hii leo Septemba Mosi, 2021, Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
"Tunafahamu kabisa Magereza kuna changamoto ya magodoro na serikali inawajibika kuhakikisha magodoro yanakuwepo, sasa haioni haja ya mahabusu au wafungwa wote wakawa na kigezo cha kwenda na magodoro yao ili waweze kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro Gerezani, kwa sababu siyo wote wanashindwa kuwa na magodoro kuliko kuiongezea serikali mzigo," amesema Mbunge Neema.