Mbunge CHADEMA aeleza machungu ya 2015

Jumanne , 12th Mar , 2019

Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Singida kupitia CHADEMA, Jesca Kishoa amesema yeye ni miongoni mwa wabunge wakike ambao ni shupavu kutokana na historia ya kumpatia ushindani wa hali ya juu Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba huku akiwa na mimba wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015.

Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Singida kupitia CHADEMA, Jesca Kishoa

Mbunge Kishoa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv iliyotaka kufahamu juu ya changamoto anazokutana nazo kama Mbunge mwanamke ndani siasa za Tanzania.

Akizungumza na www.eatv.tv Mbunge huyo amesema, "mwaka 2015 niligombea Ubunge nikiwa na ujauzito wa miezi tisa na nilijifungua kipindi cha kampeni lakini niligeuza kuwa fursa, kwa sababu nilipata huruma ya watu na chama changu."

"Changamoto nyingine wanayokutana nayo wanawake ni rushwa ya ngono kwenye siasa wengine wanaamini ili upate nafasi ya siasa lazima utoe rushwa ya ngono japo ina ukweli na ina uongo." ameongeza kishoa.

Mapema hivi karibuni Mbunge huyo alisema licha ya yeye kuwa chama tofauti na mume wake ambaye ni David Kafulila, lakini wamewekeana utaratibu kila mtu kuheshimu itikadi ya mwenzake.