Mfahamu aliyetenguliwa na kuteuliwa hii leo

Jumapili , 12th Jul , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Dkt Maduhu Isaac Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambapo kabla ya uteuzi huo Dkt Kazi alikuwa ni Meneja wa Idara za Sera za Kibajeti na Madeni wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, na kulia ni Godffrey Mwambe aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC.

Dkt Kazi anachukuwa nafasi ya Godffrey Mwambe, na uteuzi huo umeanza rasmi hii leo Julai 12, 2020.

Mei 17, 2017, Rais Magufuli alimteua Godffrey Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, ambapo kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, hivyo Mwambe amedumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu.