Jumatatu , 6th Mar , 2023

Wizara ya Elimu imepiga marufuku kwa shule kutoa huduma ya bweni kwa wanafunzi wa awali, darasa la kwanza hadi darasa la nne isipokuwa kwa kibali kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika.

Vitanda

Marufuku hiyo imetolewa na kamishna wa Elimu Dkt Lyabwene Mtahabwa, na hivyo shule zinazotoa huduma kwa watoto walio katika ngazi hizo wanatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza wa mwaka 2023.

Kamishna Dkt Mtahabwa amesema kwamba huduma ya bweni kwa watoto huwanyima fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili  na kushiriki katika shughuli mbalimbali  za maendeleo kwenye familia zao.