
Mwenyekiti wa mtaa wa Zahanati Mashaka Nkonyoka ameiambia EATV kuwa Mgogoro huo umetatuliwa na sasa kanisa la EAGT limerudishwa kama awali
‘Mgogoro ni wa muda mrefu sana hadi ulipoibuka kwa mchungaji kubadilisha jina la kanisa jipya ambalo lilileta utata huu mimi nashukuru kwa maamuzi ya kupata waumini kuendelea na ibada na kurejesha maandishi yao ya awali pia ni jambo sahihi’
Mwenyekiti huyo amesema kwa saa mtaa huo una amani na kuwataka wakazi wake kuishi bila wasiwasi wowote
‘Naomba kuwaambia waumini na wananchi wowote wa mtaa wangu hata mitaa ya Jirani suala la ulinzi hapa lipo vizuri hakuna hofu yoyote kwa muumini yoyote anayesali hapa aje kusali hakuna shaka yoyote ulinzi upo vizuri naamini na wao watakuwa salama’
Ikumbukwe kuwa mgogoro huo wa kubadilisha jina la kanisa uliozuka wiki moja iliyopita ulipelekea shughuli za ibada kusimama katika kanisa hilo na kusababisha milango yote kufungwa
Awali mchungaji wa kanisa hilo alibadilisha jina la kanisa la EAGT kuwa Assemblies Of God Gospel Church International jambo ambalo waumini hawakukubaliana nalo