Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Waziri Aweso amefikia uamuzi huo mara baada ya mbunge wa Kondoa Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Uwekezaji Dk.Ashatu Kijaji, kulalamikia utendaji kazi usioridhisha wa RUWASA katika eneo hilo na kusababisha wananchi kukosa maji safi na salama ya kutumia ,hali inayosababisha kuongezeka kwa magonjwa ya kuambukiza sambamba na kumsimamisha kazi Mhandisi huyo.
Katika hatua nyingine Mhe.Aweso na Dk. Kijaji wamewaonya nananchi kuacha kuchanganya siasa na vitu vya maendeleo vinavyofanywa na serikali.