Jumatatu , 15th Dec , 2025

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dodeoma baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji sambamba na wajumbe wengine wawili.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema kuna haja ya kubadili mfumo wa Magereza nchini ili kuendana na kasi ya dunia huku akigusia dhamira ya serikali kupitia baadhi ya sheria na kuzifanyia mabadiliko ili kuweza kuboresha masuala ya Haki Jinai.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dodeoma baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji sambamba na wajumbe wengine wawili.

Naye Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma Mheshimiwa, Dkt. Juliana Masabo amepongeza juhudi zinazoendelea katika kutoa haki kwa watuhumiwa hali inayopelekea tatizo la uchelewaji wa upelelezi kupungua.