Alhamisi , 3rd Nov , 2022

Miili kumi ya vijana wenye umri wa kati ya miaka  20 imekutwa imetelekezwa   huko nchini  Nigeria   kwenye njia ya kichaka  katika jimbo la kusini la Edo.

Taarifa za polisi wan chi hiyo zinasema kwamba miili hiyo haina alama inayoonekana ya vurugu na jamii za karibu na eneo hilo zimeshindwa kutambua vijana hao. 

 Msemaji wa polisi Chidi Nwabuzor amesema miili hiyo imepatikana katika eneo lililo mbali na barabara ya Lagos-Abuja siku ya Jumanne baada ya kugundulika  na maafisa wa polisi na wawindaji wa eneo hilo.

Chanzo vya vifo hivyo bado hakijulikani.

Miili hiyo imelepekwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti kwa ajili ya uchunguzi, na kwamba polisi wamewataka watu wawe na utulivu uchunguzi ukiendelea.