Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Milioni 250 zatengwa kwaajili ya wafanyabiashara

Jumatatu , 15th Apr , 2024

Shirika la viwango Tanzania (TBS), limewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo nchini kutumia fungu lililotengwa na Serikali shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuongeza viwango vya bidhaa zao ili kujiongezea wigo wa biashara zao kukubalika kimataifa.

Dkt Athuman Ngenya, Mkurugenzi Mkuu wa TBS

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Athuman Ngenya wakati akiongea na EATV leo jijini Dar es Salaam na kuwataka kutumia fursa hiyo kuongeza thamani ya bidhaa zao.

"Serikali imetoa fungu la shilingi milioni 250 kwa ajili ya uongezaji thamani bidhaa za wafanyabiashara wadogo ambapo kwa kufanya hivyo kunawaondolea vikwazo wanapoenda nchi yoyote ya ukanda wa Afrika Mashariki kutokutana na kikwazo chochote", Dkt. Athuman Ngenya

Aidha, katika kudhibiti mianya ya bidhaa zisizo na ubora TBS imesema inashirikikana na taasisi nyingine za Serikali kuhakikisha hakuna bidhaa bandia inaingia nchini.

"Tunashirikiana na taasisi nyingine za Serikali kama TRA, FCC, TAMISEMI, Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kwahiyo kuna muda tunaambatana nao ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini ni salama" Dkt. Athuman Ngenya

Kwa upande wao wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, wameiomba Serikali iweze kutoa elimu ya kutosha kuhusu utofauti wa bidhaa halisi na bidhaa bandia.

"Tunaiomba serikali iweze kutupa elimu ili tuweze kutofautisha kwani wengi wetu hata elimu zetu ziko chini na hatuwezi kutofautisha uhalali na ubandia wa bidhaa tunazotumia", Mariam Joseph, Mkzi wa Dar es Salaam.

"Kwenye kutofautisha hatujui sisi tukifika tunanunua tunatumia mpaka itokee madhara ndio huwa tunafuatilia" Selestine Enock, Mkazi wa Dar es Salaam.

"Uelewa wangu upo kwenye bidhaa moja tu ya maji labda utakuta umenuua chini unakuta kama imetobolewa halafu imewekewa gundi lakini kwa upande wa bidhaa nyingine sifahamu lakini natamani kuipata elimu hiyo", Almas Hassan, Mkazi wa Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala