
Waziri wa Nishati January Makamba
Waziri wa Nishati January Makamba ametoa kauli hiyo bungeni wakati akiwasilisha taarifa ya Wizara yake kuhusu namna serikali inavyoshughulikia suala la kupanda kwa bei ya nishati hiyo
"Rais ameelekeza serikali ijibane, ijinyime na zitolewe shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini, kwahiyo serikali imeamua kutoa bilioni 100 sasa kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta, Ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka huu wa fedha, na hazitagusa miradi ya maendeleo inayoendelea" aamesema Waziri Makamba katka taarifa yake
Aidha waziri huyo amesema katika hatua nyingine serikali ilianza mchakato wa kuchukua mkopo wa amsharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na shirika la fedha IMF kwa ajili ya kuleta ahueni katika bei ya mafuta ambapo amesema mchakato huo upo mbioni kukamilika
"Serikali ilianza taratibu za kuchukua mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia, na IMF, kwa ajili ya kuweka ahueni kwenye bei za mafuta na bidhaa nyinginezo zinazogusa maisha ya watanzania, mchakato upo mbioni kukamilika" amesema Makamba