Alhamisi , 17th Nov , 2022

Mke wa diwani wa Kawe jijini Dar es Salaam Mutta Rwakatare, amekiri kutokujua ni wapi alipo mume wake huyo kwani hadi sasa unakaribia mwezi wa tatu bila diwani huyo kuonekana nyumbani na kusema amechoka na tabia hizo na hatohangaika tena kumtafuta.

Diwani wa Kawe jijini Dar es Salaam Mutta Rwakatare

Hayo ameyabainisha hii leo Novemba 17, 2022, wakati akizungumza na East Africa TV & Radio digital, mke wa Mutta amesema kuwa awali alipopotea alikutwa kwenye moja ya gesti zilizopo wilayani Kinondoni akiwa na mwanamke na walifanikiwa kumrudisha nyumbani lakini baadaye alitoweka tena hadi leo.

Ikumbukwe awali diwani huyo alipotea ambapo taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilieleza kumpata akiwa nyumbani kwa Ashura maeneo ya Tabata Dar es Salaam.