Ijumaa , 30th Sep , 2022

Mkuu wa majeshi Jenerali Jacob John Mkunda amewataka askari wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania mara wanapo arodheshwa kulitumikia jeshi hilo,kuishi kulingana na kiapo chao ambacho huwakumbusha kuwa hodari ,waaminifu na watiifu.

askari wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania

Jenerali Mkunda ametoa kauli hiyo mkoani arusha katika kikosi cha jeshi 833 kj Oljoro wakati wa kufunga mafunzo ya kundi la kuruti zaidi ya 2000 ambao kwa sasa Tayari ni Askari wapya ,ambapo amesisitiza Askari hao kuiheshimu katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuishi kiapo chao muda wote.

Kwa upande wake Mkuu wa mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko Cannal Sijaona Myala wamesema,shule itaendelea kukazia mafunzo ya kijeshi kwa vitendo ili kuwajenga vizuri Askari wa Jwtz hasa katika hatua za awali