Ijumaa , 20th Mei , 2016

Mkuu wa Wilaya Mlele Kanali Mstaafu Issa Njiku, ameagiza kukamatwa kwa watu wote waliohusika katika wizi wa dawa muhimu, katika Zahanati ya Mnyamasi katika halmashauri ya Nsimbo na kusababisha baadhi ya huduma matibabu kusimama katika kituo hicho.

Mkuu wa Wilaya Mlele Kanali Mstaafu Issa Njiku

Kanali Njiku ametoa agizo hilo kwa Mkuu wa polisi wa wilaya ya Mlele, na kuagiza uchunguzi ufanyike haraka kwa watumishi na kwa raia wenye maduka ya madawa kijijini hapo.

Mkuu huyo wa wilaya huyo amemwambia Mkuu huyo wa wilaya ya Mlele achukue hatua hizo za haraka kutokana na watu hao kuiba dawa muhimu ambazo zinahitajika kwa ajili ya matibabu katika kijiji hicho kwenye Zahanati hiyo kubwa inayotegemewa na watu wengi katika kijiji hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Mlele ameitaka jamiii nzima itoe ushirikiano kwa jeshi hilo ikiwemo kutoa taarifa za siri juu ya watu wanafanya matukio mbalimbali kijijini hapo ikiwemo waliohusika na wizi huo.

Baada ya kutonekana kwa dawa muhimu katika Zahanati hiyo ndipo Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo ametaka kufungwa kwa kituo hicho kutokana na wizi huo wa dawa ambazo zimesababisha wagonjwa wengi kukosa huduma stahiki.