Mlinzi asimulia alivyomuua mwanafunzi

Jumanne , 16th Apr , 2019

Mshitakiwa, Hamis Chacha anadaiwa kukiri kumpiga kwa ubapa wa panga na kisha kumuua mwanafunzi Humphrey Makundi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mkoani Kilimanjaro, mwezi Novemba 2018.

Polisi wakifukua mwili wa mwanafunzi ambao ulizikwa na jiji

Katika maelezo hayo yaliyopokelewa mahakamani  kama kielelezo namba P8, mshitakiwa aliyekuwa mlinzi, anadaiwa kukiri kuua, lakini amedai hakufahamu kuwa aliyemuua ni mwanafunzi wa shule hiyo.

Mbali na kudaiwa kutoa maelezo hayo, lakini mshitakiwa anadaiwa kueleza alivyowasiliana usiku huo kwa simu na mshitakiwa wa pili, Edward Shayo ambaye ndiye mmiliki wa shule ya Scolastica, aliyetoa wazo la mwili kutupwa mtoni, na mshitakiwa wa tatu Laban Nabiswa.

Mlinzi aliandika maelezo yote yaliyosomwa mahakamani 

 

Shahidi ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Moshi Mjini, alidai aliandika maelezo hayo Novemba 20, 2017 baada ya mshitakiwa kukubali kwa hiyari yake kutoa maelezo bila kushurutishwa. Maelezo hayo yalisomwa mahakamani.

Akisoma neno kwa neno katika maelezo hayo, shahidi huyo amemnukuu mshitakiwa akieleza kuwa Novemba 6, 2017 saa 2:58 usiku, alisikia kishindo cha mtu akishuka (ukuta) na aliamua kufuatilia, na alipomulika tochi kuelekea eneo hilo, mtu huyo alianza kukimbia na yeye alimkimbiza kwa vile alikuwa na silaha aina ya panga, ambalo alimpiga nalo kwa ubapa.

“Nilimpiga bapa mgongoni na aliendelea kukimbiana nikakimbizana naye, kuna sehemu alifika na kuanguka chini na alipasuka kwenye paji la uso. Baada ya hapo akawa katulia. Nikampiga bapa la pili na ndio mauti yalipomkuta pale pale”.

“Nilimpigia simu mwalimu Laban nikamwambia kuna mtu nimemkimbiza lakini sijui kama ni mwanafunzi au mtu wa nje. Ndipo mwalimu Laban ambaye ni mwalimu wa nidhamu akaja. Palepale akaniuliza nimeshampigia mkuu wa shule nikamjibu nishampigia, mzee wa shule Mzee Shayo anakuja. Baada ya hapo nilimwambia mwalimu Laban inawezekana huyu mtu kazirai tumbebe tumpeleke hospitali, mwalimu Laban akadai tumsubiri Mzee Shayo. Mzee Shayo alivyofika ndio nikamueleza.”, ameeleza shahidi huyo akisoma amelezo ya mshtakiwa namba moja Chacha.

“Mzee Shayo akamuuliza mwalim Laban, unamfahamu huyu mtu, Laban alijibu naona kavaa sare za shule lakini siwezi kumfahamu kwa muda huu. Mzee Shayo akasema kama humfahamu kwa muda huu akatupwe mtoni labda ni kibaka na mimi na mwalim Laban tulienda kumtupa mtoni”.

“Jumatano kuamkia Alhamisi ndio wakampigia simu mzazi. Nilikuja kukamatwa siku ya Ijumaa saa 11 jioni nikiwa lindo shuleni Scolastica na tulipelekwa kituoni Himo.”

“Tulikaa pale kuanzia saa 11 hadi saa 1 usiku tukapelekwa Central Police Moshi mjini na kufika kituoni walinipiga polisi wengi ili nitoe maelezo sababu nilitofautiana na mlinzi mwenzangu. Hadi leo tarehe 20.11.2017 niliomba mwenyewe kuja kutoa maelezo kwa mlinzi wa amani. Nakiri kuwa nimeua lakini sikufahamu kabisa kama yule alikuwa mwanafunzi wa pale Scolastica”.

Mwili wa mtoto huyo uliokotwa Novemba 10, katika Mto Ghona, mita zipatazo 300 kutoka shuleni hapo, na polisi waliouchukua waliupeleka Hospitali ya Mawenzi na kuzikwa kwa madai haukutambuliwa.

Ushahidi wa Vinasaba (DNA) ambao ushapokelewa mahakamani kama kielelezo cha kesi hiyo, ulithibitisha kuwa mwili huo una vinasaba na Jackson Makundi na Joyce Makundi ambao ni wazazi