Jumatatu , 30th Mar , 2020

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte, amefariki Dunia Alfajiri ya leo ya Machi 30, 2020, mauti hayo yamemfika akiwa kwenye Taasisi ya mifupa MOI alipokuwa akipatiwa matibabu.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte, wakati wa uhai wake.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, Msemaji wa taasisi hiyo, Patrick Mvungi, amesema kuwa Shamte walimpokea Machi 23, na baadaye hali yake ilibadilika na wakamuhamishia kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU).

"Ni kweli Shamte amefariki dunia Alfajiri saa 12:44 asubuhi, tulimpokea Machi 23 na baadaye hali yake ilibadilika na Machi 26 tukamhamishia chumba cha uangalizi (ICU) na hatimaye leo asubuhi akawa amefariki" amesema Mvungi.