Alhamisi , 5th Dec , 2019

Mahakama ya Wilaya ya Ifakara, mkoani Morogoro, imemuhukumu kutumikia kifungo cha mwaka 1 jela au faini ya shilingi Milioni 2 pamoja na kuviteketeza viuatilifu kwa gharama zake mwenyewe, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yerusalem Mwamaja (49), baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa

Mahakama ya Wilaya ya Ifakara, mkoani Morogoro.

na viuatiliafu visivyosajiliwa.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Binge Njaga Mashabara, baada ya kujiridhisha na hoja za mashahidi watatu wa upande mashtaka, bila kuacha shaka yeyote.

Hakimu Mashabara amesema, vitendo kama hivyo vinawasababishia hasara wakulima na Serikali kwa ujumla ukiachilia mbali kuendelea kusababisha madhara kwa mazingira na kwa Afya za binadamu, wanyama na mimea.

Katika utetezi wake Yerusalem Mwamaja alikubali mashtaka na aliomba apunguziwe, adhabu kwani ni mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho na hata rudia.