Jumapili , 5th Jul , 2020

Vibanda zaidi ya 7 vya maduka ya wafanyabiashara katika soko la Vwawa wilayani Mbozi Mkoani Songwe vimeteketea kwa moto. 

Picha hii sio ya tukio la leo

Taarifa za awali zimeeleza kuwa moto huo umezuka alfajiri ya leo Julai 5, 2020 na kuteketeza maduka hayo ndani ya soko.

Mpaka muda huu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea na jitihada za kuuzima moto huo.

Chanzo bado hakijabainishwa na jitihada za kuwapata watu wa mamlaka za usalama zinaendelea.