
Muonekano wa Maduka yaliyoteketea kwa moto.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka aliongoza wananchi kuzima moto huo ambao uliibuka saa 5 na dakika 20 usiku katika moja ya duka la nguo na kusambaa katika maduka mengine ya bidhaa za vyakula, hoteli, stoo za vifaa vya ujenzi, salooni na maduka ya bidhaa mchanganyiko.
Mheluka amesema kuwa chanzo cha moto huo hakijafahamika mpaka sasa.