
Juhudi hiyo inafanyika wakati Rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa kundi la wapiganaji wa Kipalestina liko tayari kufanya maridhiano kuhusu mapendekezo yake ya makubaliano ya amani. Kwa faragha na chini ya ulinzi mkali, wajumbe walitarajiwa kuzungumza kupitia wapatanishi kati ya pande hizo, ikiwa ni wiki chache tu baada ya Israel
kujaribu kuwaua wajumbe wakuu wa Hamas katika shambulio huko Qatar. Taarifa ilisema "Upatanishi wa Misri na Qatar unafanya kazi na pande zote mbili kuanzisha utaratibu wa kuwaachilia mateka walioko Gaza kwa kubadilishana na Wapalestina walioko magerezani Israel.
Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kuwa alikuwa na uhakika kiasi kuwa makubaliano ya amani yanawezekana. Merz aonya kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi Katika kumbukumbu ya miaka miwili tangu mauaji ya Oktoba 7 yaliyofanywa na kundi la Hamas nchini Israel, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa Hamas na Israel kusitisha vita vya Gazamara moja. Akisema pendekezo jipya la Rais Trump linatoa fursa ya kumaliza mgogoro huo.
Aidha katika kipindi cha kumbukumbu hiyo pia Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ameonya kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani.