Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mpenzi wako anavyoweza kukupa vidonda vya tumbo

Jumanne , 31st Jul , 2018

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuna asilimia kubwa ya watu wanaoumwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo, wanaweza kuwasababishia wapenzi wao ugonjwa huo endapo watakuwa wanafikiria sana juu ya ugonjwa huo anaoumwa mpenzi wake.

Mtu mwenye maumivu makali ya tumbo ambayo yamesababishwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango katika mradi wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele kitaifa kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Oscar Kaitaba wakati alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv na kusema, chanzo cha ugonjwa huo ni 'acid' nyingi inayozalishwa kutoka kwenye mwiili wa binadamu, baada ya kuwepo na hasira, mawazo pamoja na ukosefu wa mlo kamili.

"Vidonda vya tumbo haviambukizi kama watu wanavyosema huko mitaani, ila mtu anaweza kupata vidonda hivyo ikiwa yupo na mpenzi wake, mume au mke halafu akawa na mawazo ya kumfikiria kama atapona au atakufa, na kusababisha na yeye kuumwa ugonjwa huo kutokana na mawazo aliyokuwa nayo pamoja na kushindwa kula vizuri lakini sio kwamba inaambukiza moja kwa moja", amesema Dkt. Kaitaba.

Pamoja na hayo, Dkt. Kaitaba ameendelea kwa kusema "muda mwingine sababu za kiuchumi, mawazo na hasira huwa inasababisha kutengeneza 'acid', na 'acid' ikiwa nyingi mwilini ndipo inapochimba utumbo na kupelekea mtu kujikuta katika ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Vidonda vya tumbo vinatibika kabisa ila cha msingi mgonjwa anapaswa kwanza kukutana na wataalamu wa afya kabla ya kuanza kutumia dawa ya aina yoyote".

Dkt. Oscar Kaitaba ameeleza hayo baada ya kuwepo tetesi kwenye jamii ya kitanzania kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo huweza kumuambukiza mtu kwa kutumia vitu ambavyo mgonjwa anavitumia kama kikombe na vitu vingine.

Msikilize hapa chini Dkt. Oscar Kaitaba akielezea zaidi juu ya ugonjwa huo na tiba yake

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita