
Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP) na Mwenyekiti wa bodi ya Parole Agustino Mrema.
Kwa mujibu wa Mrema maazimio hayo si mara kwanza kwa vyama vya upinzani nchini kuyafikia lakini yamekuwa hayana matokeo kutokana na kutokuwa na umoja baina ya vyama vya siasa nchini.
Akizungumza na www.eatv.tv amesema "haya maazimio waliyoyatoa ni kwao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma japo baadaye walitofautiana kuyatekeleza, mimi siamini kama yatafanikiwa kwa sababu hawana umoja."
"Mfano mzuri mimi kule Vunjo walinitenga, wakaacha kupambana na CCM wakaanza kupambana na mimi ili wanitoe na wakafanikiwa kunitoa na athari zake zinaonekana kwa sababu Vunjo sio ngome ya upinzani tena."
Mrema alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambaye alijibebea umaarufu kwa utendaji kazi wake lakini pia alishawahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo ambapo mwaka 2015 kiongozi huyo alienguliwa na Mbunge wa sasa James Mbatia.