
Miraji Mtaturu ameapishwa na Spika Job Ndugai, wakati wa kuanza kwa kikao cha kwanza mkutano wa 16, wa Bunge la 11, ambapo baada ya kuapishwa Miraji Mtaturu pia alipata nafasi ya kuuliza swali kwa mara ya kwanza.
"Namshukuru Mungu kwa kunijaalia kuingia kwenye Bunge hili tukufu, kuwawakilisha wananchi wa Singida Mashariki, Jimbo la Singida Mashariki, na Wilaya ya Ikungi ina tatizo la maji, na kuna visima vimeshaanza kupimwa, tunahitaji Bil. 2" amesema Miraji Mtaturu.
Akijibu maombi hayo Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso, amemtaka Mbunge huyo kukutana ili kujadili namna ya kumaliza tatizo hilo.
"Nimuombe baada ya Bunge saa 7 tukutane tujadili namna ya kumaliza tatizo la maji." amesema Naibu Waziri Aweso.
Hivi sasa kuna kesi inayoendelea Mahakama Kuu ya Tanzania, kuhusiana na taratibu zilizotumika kumvua Ubunge Tundu Lissu.