Jumatatu , 1st Mar , 2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi, amemteua Othman Masoud Othman Sharif, kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Othman Masoud Othman Sharif, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar mteule

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Machi Mosi, 2021, na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said, na kueleza kuwa uteuzi huo umeanza leo na ataapishwa kesho Machi 2, Ikulu Zanzibar.

Othman Masoud Sharif, anachukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki dunia Februari 17 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa uteuzi huo umefanyika baada ya kushauriana na Chama cha ACT-Wazalendo.