Alhamisi , 17th Oct , 2019

Msanii wa muziki wa Injili nchini Joel Lwaga, amesema moja ya wanasiasa ambao wanamvutia sana kwenye medani za siasa Tanzania ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, na kusema kama yeye asingekuwa muimbaji wa muziki malengo yake angekuwa mwanasiasa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni, kinachorushwa kupitia kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Lwaga amesema zamani alitamani sana kuwa mwanasiasa, ila familia ikamfanya aingie kwenye dini.

"Ukiniuliza kwa sasa kwenye medani za siasa nchi nzima nampenda nani hakuna asiyejua mwanasiasa anayevutia kwa sasa ni Rais John Pombe Magufuli, japo mwenyewe huwa hajiiti mwanasiasa" amesema Joel Lwaga

"Halafu unajua mimi rafiki zangu wengi walidhani mimi ningeweza kuwa mwanasiasa kwa sababu kila ngazi niliyokua napita nilikuwa nakuwa kiongozi wa ngazi fulani" ameongeza Joel Lwaga.

Aidha katika kipindi hicho msanii alipoulizwa kuhusiana na je yeye ni mfuasi wa chama gani cha siasa alisema yeye ni mpenzi na mshabiki mkubwa wa Tanzania.

Tazama mahojiano kamili hapo chini.