Jumanne , 9th Apr , 2024

Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) imekabidhi bidhaa za afya mbalimbali kwa waathrika wa mafuriko Wilayani Rufiji mkoani Pwani

Bidhaa hizo zimekabidhiwa  kituo cha Afya Mohoro kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji  ambazo ni pamoja na Dawa, za kuzuia  na kutibu malaria, kuhara na yale ya mlipuko kama vile kipindupindu. 

Kwa upande wa vifaa tiba ni pamoja na  magodoro, mashuka na vyandarua, milingoti ya kutundikia maji tiba ( Drip Stand), Binliners na vifaa vingine vitakavyosaidia katika zoezi hili. 

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa bidhaa hizo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Dr. Hamis Abdallah.

ameishukuru MSD kwa juhudi  za haraka zilizofanyika kuweza kuwafikia wahanga wa mafuriko. Ameongeza kuwa bidhaa hizo zitasaidia katika utoaji wa huduma kwa waathirika wa mafuriko. #EastAfricaTV