Msigwa afanya utafiti ili kujua anavyopendwa

Jumatano , 12th Feb , 2020

Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, amesema kuwa amefanya utafiti wa mwezi mmoja na kubaini kuwa kati ya wananchi 10 jimboni mwake 7 kati ya hao wanamkubali na wanataka aendelee kwenye nafasi yake ya Ubunge.

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa

Akizungumza leo Februari 12, 2020, na EATV&EA Radio Digital, Mchungaji Msigwa amesema kuwa bado anayo nia ya kuendelea kuongoza jimbo la Iringa Mjini na kwamba wananchi bado wana muhitaji sana.

"Katika research niliyofanya katika watu 10, 7 kati yao wananiunga mkono, wawili wanaiunga mkono CCM, Mmoja haelewi na hajafanya maamuzi, sasa nitakosaje kugombea na nimelipa hela nyingi sana ili kufanya utafiti kitaalamu" amesema Msigwa.

Tazama Video hapa chini.