Jumanne , 13th Dec , 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene, ametoa rai kwa wananchi wa Mtera kuacha kutumia nyavu haramu katika shughuli zao za uvuvi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene

Wito huo ameutoa katika mkutano wa hadhara aliofanya Kata ya Mtera, jimbo la Kibakwe  Halmashauri ya wilaya ya  Mpwapwa uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

"Msitumie nyavu za timba, ambazo zina sumu, ambazo zinauwa mazalia ya samaki na hata kwa mtumiaji wa samaki waliovuliwa kwa nyavu hizo anaathirika," ameelekeza Waziri Simbachawene

Naye afisa Uvuvi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Fransisco Mwanga amesema uvuvi wa kutumia nyavu haramu aina ya timba ni hatari, madhara yake inapogusana na samaki ni kushindwa kuzaliana na kwamba elimu imetolewa kwa wavuvi na wakati mwingine kupigwa faini lakini bado wameendelea na uvuvi haramu uliosababisha samaki kutozaliana.