Alhamisi , 15th Nov , 2018

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea ametangaza kujivua nafasi yake ya ubunge kupitia Chama Cha Wananchi CUF kwa kile alichokieleza juu ya uwepo kwa mgogoro wa kiuongozi baina ya pande mbili za viongozi wa Chama hicho ikiwemo upande wa Lipumba na Maalim Seif.

Aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.

Mtolea ametangaza uamuzi Bungeni Jijini Dodom wakati wa muendelezo wa vikao vya Bunge la mkutano wa 13 kikao cha 7, ambapo majira ya saa saba kasoro mchana kabla ya wabunge hawajaenda mapumziko Mtolea alitangaza uamuzi huo.

www.eatv.tv imejaribu kumtafuta mbunge huyo lakini hakupatikana kwa njia ya simu ila kupitia waliokuwa watu wake wa karibu ambaye ni Mbunge Selemani Bungara maarufu kama Bwege alithibitisha kujiuzulu kwa mbunge huyo ndani ya bunge.

Ni kweli Mtolea ajiuzulu na hilo limetokea kama leo bungen dakika chache zilizopita na sababu zake kubwa anadai kuwa Chama kina mgogoro, lakini hakutangaza anajiunga na chama gani,” amesema Mbunge Bwege.

Novemba 15 mwaka huu Chama Cha Mapinduzi kilitangaza kuwa ndiyo siku ya mwisho ya Chama hicho kupokea wabunge na madiwani ambao wanahitaji kujiunga na baadaye kupewa nafasi ya kugombea tena nafasi yake ya awali.

Mtolea anakuwa mbunge wa kumi kutoka vyama upinzani ambao wameshahama vyama vyao kutokana na sababu mbalimbali