Ijumaa , 3rd Dec , 2021

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, limefanikiwa kumuokoa kutoka ndani ya shimo la choo cha shule, mtoto mchanga wa kiume mwenye umri wa kati ya siku mbili hadi tatu aliyetupwa katika shimo hilo na mtu ambaye hajafahamika, akiwa amefungwa kwenye mfuko.

Mtoto aliyeokolewa ndani ya shimo la choo akisafishwa

Kaimu Mkuu wa Jeshi hilo mkoa wa Kagera, Thomas Majuto, amesema kuwa mtoto huyo alitupwa katika shimo la choo cha shule ya msingi Rukanyange Desemba 01 mwaka huu na kwamba walipopata taarifa walifika haraka eneo la tukio na kufanikiwa kumwokoa akiwa hai.