Mama wa mtoto aliyelawitiwa
Mama wa mtoto huyo anasema kuwa baada ya kutoa taarifa kituo cha Polisi ambaoi mtuhuhumiwa alikamatwa lakini baadae akaachiwa huru huku akitishia usalama wa mtoto huyo.
"Mwanangu alikuwa anatoa harufu za ajabu nilipomchunguza nikagundua ameingiliwa kinyume na maumbile na nilipomuuliza akagoma kusema lakini baada ya kumpiga akasema mama naogopa nitakufa kwa maana aliyenifanyia amesema nikisema ataniua, nikatoa taarifa Polisi lakini nashangaa mtuhumiwa ameachiliwa huru huku akitoa vitisho", Mama wa mtoto.
Aidha ameomba wasamaria wema wamsaidie kupata matibabu ya mwanaye kwani tangu akutwe na tukio hilo hajatumia dawa yeyote.
"Naomba wasamalia wema wanisaidie mimi ni muuza vitafunwa sina uwezo wa kugharamia matibabu ya mwanangu kwani tangu akutwe na tukio hajameza hata panadol kutokana kiasi kidogo alichonacho anakitumia kwa ajili ya kula", Mama wa mtoto.
Kutokana na kutishiwa amani imemlazimu kukimbia Kibaha kwa ajili ya usalama wake na mtoto wake.
"Niliongea na diwani nikamwambia changamoto nayopitia akanipa namba ya mtendaji nilipompigie mtendaji akanambia kwahiyo tufanyaje tukupe askari na bunduki akae na wewe nyumbani kwako nikamjibu kipole tu, kwahiyo sina mahali pa kukaa nikisaidiwa na makazi nitafurahi sana", Mama wa mtoto.