Jumatatu , 6th Oct , 2025

Rashid Lugwisha, Daktari kutoka hospitali ya Manispaa ya Geita pamoja na Jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuruhusu ndugu na jamii kuendelea na taratibu za maziko kutokana na mwili wa marehemu kuharibika vibaya huku wakiendelea na uchunguzi kuwatafuta waliousika na kifo chake.

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba (7) anayefahamika kwa jina la Magreth Dickson mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kalangalala, amekutwa amefariki dunia ikiwa ni siku sita zimepita tangu aripotiwe kupotea nyumbani alikokuwa akiishi na bibi yake katika eneo la Katoma, kata ya Kalangalala manispaa ya Geita.
 
Vilio na majonzi vimetawala kwa familia ya mtoto huyo aliyekuwa anaishi na bibi yake Bi.Salma Mrisho ambapo siku ya jumatatu septemba 29 2025 mtoto huyo hakurudi nyumbani baada ya kumuaga Bibi yake kuwa anaenda kucheza na watoto wenzake.

Bibi alipoona imefika saa mbili usiku mtoto hajarudi nyumbani alitoa taarifa kwa uongozi wa mtaa.

Rashid Lugwisha, Daktari kutoka hospitali ya Manispaa ya Geita pamoja na Jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuruhusu ndugu na jamii kuendelea na taratibu za maziko kutokana na mwili wa marehemu kuharibika vibaya huku wakiendelea na uchunguzi kuwatafuta waliousika na kifo cha mtoto huyo.