
Balozi wa Tanzania nchini Japan Baraka Luvanda
Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 7, 2022, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya kwa njia ya mtandao.
"Japan pamoja na nchi zingine ninazozifahamu, suala la kodi halina masihara hata kidogo, hakuna tabia ya kutokulipa kodi na mtu kama ametenda kosa la kukwepa kodi yuko tayari hata kujitoa uhai, sababu wanaamini maendeleo yanatokana na kodi, mchango wa kodi ni mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa lolote, utamaduni huu kwa kweli tungeiga tungefika mbali," amesema Balozi Luvanda.
Aidha Balozi Luvanda akatoa wito kwa Watanzania, "Wale wanaopinga masuala ya tozo (Tanzania) nadhani wapate tafakari pana zaidi, Japan hakuna ukwepaji wa kodi na kuna tozo mbalimbali na watu wanaheshimu, na kodi ndizo zinaendeleza hizi nchi,".