Ijumaa , 15th Jan , 2021

Mgombea urais wa Uganda kupitia chama cha NRM, Yoweri Museveni, anaongoza kwa kura nyingi katika matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya nchini humo, yaliyotangazwa mapema asubuhi ya leo ya Januari 15, 2021.

Mgombea urais wa Uganda, kupitia chama cha NRM, Yoweri Museveni

Tume ya Uchaguzi nchini humo imetangaza kuwa Yoweri Museveni, amepata kura 1,536,205, sawa na asilimia 65.02, huku mpinzani wake Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, akipata kura 647,146, sawa na asilimia 27.39%, matokeo hayo ni kutoka katika vituo 8,310.

Uganda ina jumla ya vituo 34, 684 vya kupigia kura.

Aidha zoezi la uhesabuji wa kura, katika kituo cha kitaifa cha majumuisho ya kura zote linaendelea, hadi pale mshindi atakapopatikana.

Yoweri Museveni anawania nafasi ya urais kwa aili ya kuongoza Taifa la Uganda kwa awamu ya sita sasa.