Museveni azungumzia demokrasia nchini Uganda

Jumatano , 12th Mei , 2021

Rais Yoweri Museveni ameapishwa rasmi leo Mei 12, 2021 kuwa Rais wa Uganda kwa muhula mwingine mara baada ya kushinda uchaguzi wa Januari 14, 2021.

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akila kiapo leo , Mei 12, 2021

Rais Museveni anaiongoza nchi ya Uganda kwa muhula mwingine tena, na huu ukiwa ni muhula wake wa sita tangu alipoingia madarakani mwaka 1986,  kwa mapinduzi ya kijeshi.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa Rais Museveni amesema hawatoitilia maanani mihadhara inayohusu suala zima la demokrasia ya nchi hiyo kutoka katika nchi za kigeni bali ile inayotoka barani  Afrika

Pia Rais Museveni amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu Sukari kutoka nchini humo kuingia Tanzania huku akisema kuwa kwasasa Uzalishaji bidhaa nchini Uganda ni mkubwa.

Zaidi ya marais 10 kutoka Mataifa mbalimbali wameshiriki shughuli ya uapisho huo, akiwemo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.